Siku moja nilienda bank kwa ajili ya kufungua account, siku
hiyo nilipanga kumaliza kila kitu kinachohusiana na kufungua account hiyo maana
nilikuwapo katika bank hiyo siku mbili tofauti za nyuma kwa ajili ya
kushughulikia account hiyo bila mafanikio.
Siku hiyo nilitoka nyumbani kwa kusudi moja tu la
kuhakikisha nimefanikiwa kufungua account,maana nilibeba kila ambacho
kingehitajika kuifungua account hiyo,tofauti na nilivyozoea kukuta watu
wachache na kupata huduma haraka, siku hiyo watu walikuwa wengi na mhudumiaji
counter alikuwa mmoja tu;nilibadilisha mapozi yote ya ukaaji na usimamaji ili
kuvuta muda kwa ajili ya kupata huduma,nilisubiri na kusubiri nakusubiri bila
mafanikio yoyote,
Nilifika pale asubuhi mida ya saa nne lakini mpaka wanakula
chakula cha mchana mimi bado nipo tu,mpaka inaanza kuingia saa tisa mimi bado
nipo tu…jambo moja nakumbuka nilijiambia ni kwamba “leo siondoki mpaka nimekamilisha zoezi hili”
Kuna wakati ilionekana kama sitaweza kufanikiwa kufungua
account ile kwa sababu za kisheria, ulianza mjadala wa sheria inasemaje juu ya
uanzishwaji na uendeshaji wa account ile niliyokuwa naitaka,mara zote nilikuwa
na kicheko moyoni nikijua fika kwamba sijawahi kutumia muda wangu namna hii
halafu nikashindwa,moyoni mwangu niliamini kabisa kwamba ningeweza kupata
huduma ile na kukamilisha siku hiyohiyo.
Baada ya yote hayo, wakati inaelekea saa kumi faili langu
likaanza kushughulikiwa kwa haraka maana hata watu walikuwa wamepungua,kwakufupisha
stori ni kwamba nilifanikiwa kufungua
account ile na kuanza kuweka pesa siku hiyo hiyo kama ilivyohitajika.
Ikawa siku nyingine tena Wakati nikiwa kwenye basi la
mwendo kasi nikiwa natokea posta mida ya saamoja jioni, nikiwa kwenye basi,
kuna kituo basi lilisimama ili kuchukua abiria hali ya kuwa basi lilikuwa
limejaa sana, baadhi ya abiria walianza
kulalamika kwamba dereva asifungue mlango maana basi lilijaa sana, wakati
dereva akiwa amefungua milango na watu kuanza kuingia hivyohivyo nilibahatika
kumuona mama mmoja ambaye alionekana kungangana kuingia japokuwa mwanaume mmoja
aliyesimama mlangoni alionekana kabisa kumpinga asiingie kwa kumuwekea kikumbo
na kumsukumizia nje…kwakuwa mimi nilikuwa karibu na Yule kaka niliona mchezo
mzima unavyoendelea,chakushanganza ni kwamba niliona Yule mama akiendelea
kungangania gari lile na hatimae wakati gari linaanza kuondoka na yeye alikuwa
mmoja wa wasafiri tuliokuwa nao.
Kuna kitu cha kujifunza kutoka katika habari hizi mbili
ambazo zinatukumbusha kile alichosema Yesu kwenye Biblia kwamba atakayevumilia
mpaka mwisho ndiye atakayeokoka,
Swali langu kwako leo
ni ,Je umeweza kuvumilia pale ulipoona kama ndoto yako inafifia, uliendelea
kukazana kupambana maono yako yathibitike au uliachia ngazi na kukata tamaa?
Nakukumbusha leo kuendelea kupambana mpaka tone la mwisho
kuhakikisha unafikia mwisho mwema ulioandaliwa na Mungu,usikate tamaa njiani,Be
strong.
Anza
sasa.
Hii ni kweli kabisa, na nimeiona inatokea kwangu mara nyingi sana.
JibuFutaUkivumilia mpaka mwisho utapata unachotaka.