Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2017

KUFANIKIWA KIMAISHA.

                                                      MAFANIKIO YA KIMAISHA Ili maisha yangu yawe vile Mungu anataka niwe imenipasa kuwa na nidhamu, kuna maeneo kadhaa ambayo napaswa kuweka bidii ya nidhamu katika hayo,maeneo kama;Mahusiano na Mungu,muda,pesa pamoja na kazi ni vitu ambavyo lazima niviangalie kwa jicho la pekee ukizingatia kwamba ni maeneo nyeti yatakayonipelekea kufikia malengo kama nikiyatendea kwa ustadi. Kama alivyosema kaka Fela Duratoye katika moja ya semina alizokuwa mzungumzaji juu ya jinsi ya kwenda mbele kwa kasi,alisema inabidi mtu aone ni jinsi gani anaweza kuona vitu vya; ·          Kuanza kufanya ·          Kuacha kufanya ·          Kufanya zaidi ·          Kupunguza kufanya.             Ili ufanikiwe kimaisha ni jambo la busara kujua ni mambo gani ya kuyaanza, yapi ya kuyaacha na pia yapi ya kufanya zaidi na yapi ya kupunguza kufanya. Duniani kuna mambo mengi, bila  kuwa makini unaweza kujikuta unajihusisha na kila kitu haliyakuwa muda