KUFANIKIWA KIMAISHA.
Ili
maisha yangu yawe vile Mungu anataka niwe imenipasa kuwa na nidhamu, kuna
maeneo kadhaa ambayo napaswa kuweka bidii ya nidhamu katika hayo,maeneo
kama;Mahusiano na Mungu,muda,pesa pamoja na kazi ni vitu ambavyo lazima
niviangalie kwa jicho la pekee ukizingatia kwamba ni maeneo nyeti
yatakayonipelekea kufikia malengo kama nikiyatendea kwa ustadi.
Kama
alivyosema kaka Fela Duratoye katika moja ya semina alizokuwa mzungumzaji juu
ya jinsi ya kwenda mbele kwa kasi,alisema inabidi mtu aone ni jinsi gani anaweza
kuona vitu vya;
·
Kuanza kufanya
·
Kuacha kufanya
·
Kufanya zaidi
·
Kupunguza kufanya.
Ili ufanikiwe kimaisha ni jambo la
busara kujua ni mambo gani ya kuyaanza, yapi ya kuyaacha na pia yapi ya kufanya
zaidi na yapi ya kupunguza kufanya.
Duniani
kuna mambo mengi, bila kuwa makini
unaweza kujikuta unajihusisha na kila kitu haliyakuwa muda ulionao ni
mchache,mwisho wa siku unajikuta umefanya mambo mengi lakini hayana faida
yoyote sio tu kwako bali na kwa jamii inayokunzunguka,Itambulike wazi kuwa kila
mtu aliyezaliwa mara ya pili ni nuru,kwa lugha rahisi kila aliyezaliwa mara ya
pili ni suluhisho la tatizo Fulani,
Kuokoka pekee hakutoshi,lazima ukue
na kujua sababu ya wokovu wako ndivyo ilivyo na kuzaliwa,kuzaliwa pekee
hakutoshi,lazima ufike mahali pa kujua kwanini umezaliwa ili uanze kuiishi kwa
ukamilifu sababu ya kuzaliwa kwako.
Nilisoma
mahali mwanafalsafa mmoja aliandika kuwa dunia ni ya ajabu sana si kwasababu ya
watu wanaotenda maovu bali ni ya ajabu kwa sababu ya watu wanaowatazama
wanaotenda maovu na kuwaacha hivyohivyo.
Je kuna jambo la msingi ambalo mpaka
unaingia kitandani leo unaweza kusema kuwa umelifanya? Kuna watu wa aina mbili
huku Duniani,
- Wanaofanya vitu vitokee
- Wanaotazama vitu vikitokea.
Wewe
upo katika kundi gani kati ya hayo mawili tajwa hapo juu? Kama haufanyi mambo
yatokee ujue tayari unaingia kundi la wanaotazama yanayotokea, huu sio wakati
wa kujifariji, huu ni wakati wa kuonesha ulimwengu kuwa umekataa kufa na lulu
uliyokujanayo huku duniani,
Utajisikiaje kama siku unaingia
mbinguni na kuoneshwa picha ya ulivyotegemewa kuwa na uneshindwa kuwa na
ukaoneshwa namna ambayo ungeweza kabisa kufikia kusudi la kuumbwa kwako
katikati ya changamoto ulizokuwa unapitia; amua leo kuishi vile ulivyokusudiwa
kuishi huku chini ya jua,Maisha ya kifalme na kikuhani.
Kama
ningeambiwa kufupisha ujumbe huu kwa maneno mawili ningekwambia;
#ANZASASA.
Ukishajua umekuja duniani kufanya nini,anza kufanyia kazi.
JibuFuta